Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
WARUMI 6:12-13
Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake. Wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.
WAGALATIA 5:17 inasema
Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
Mpendwa, jihadahari sana na matakwa ya mwili, ukimuachia mwili nafasi, atadhulumu Roho, maana mwili hushindana na Roho. Kumbuka ni Roho ndiyo itaenda mbinguni na ni Roho ndiye atakaye ukumiwa, si mwili. So ndiyo sababu lazima Paulo mitume anawaandikia barua kanisa la Wagalatia katika kitabu cha WAGALATIA 2:20 akisema; "Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imaniya mwana wa Mungu, ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.
Ukitaka dhambi isitawale ndani yako, lazima umwuwe mwili pamoja na tamaa zake,ili uishi matakatifu, maisha inayompendeza Mungu.
WARUMI 8:13 Inasema;
Kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa ; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.
Waumini katika Kristo Yesu wanayo asili mbili; ya kwanza ni asili ya kale ya dhambi(mwili) na asili yetu mpya ya Roho ambayo tulimpokea tulipo amini kwa Injili takatifu.
2 WAKORINTHO 5:17 Inasema;
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; yakale yamepita tazama! yamekuwa mapya.
WAGALATIA 5:16 Inasema
Basi nasema , enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili
Cha maana sasa, ni kuendelea kutembea chini ya nguvu na ulinzi wa Roho Mtakatifu. Ukiruhusu Roho achukuwe usukani katika maisha yako, Mungu atatawala ndani yako, wala hautakuwa na tamaa ya mwili tena, baali tutakuwa na shauku la kumtumikia Mungu na kufanya mapenzi yake. WARUMI 12:1-2
ENDELEA KUTAZAMIA YESU KRISTO, MWANZILISHI NA MKAMILISHI WA IMANI YETU