Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Roho Mtakatifu ndiye msaidizi wa kweli. Mtu akimpokea Kristo Yesu kuwa bwana na wokovu wake, anaitaji Roho Mtakatifu, maana ni Roho Mtakatifu huyo anaye patiana kipawa na kututia nguvu ya kufanya kazi ya Mungu.
YOHANA 14:15-16; (15). Mkinipenda, mtazishika amri zangu. (16) Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele.
< > ROHO MTAKATIFU ANASAIDIA WATEULE KUELEWA MAANDIKO:
LUKA 24:45; Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.
YOHANA 14:26; Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
< > ROHO MTAKATIFU ANASAIDIA WATEULE KATIKA MAOMBI:
Hauwezi kuomba ipasavyo, bila mwongozo wa Roho Mtakatifu, kwa kuwa ni Roho Mtakatifu ndiye anatufunulia jambo lakuombea, WARUMI 8:26; Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaivu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinzi itupasavyo, Lakini Roho mwenyewe utuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
< > ROHO MTAKATIFU ANASAIDIA WATEULE KUISHI MAISHA MATAKATIFU:
WAGALATIA 5:16; Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtatimiza kamwe tamaa za mwili.
< > ROHO MTAKATIFU ANASAIDIA WAUMINI KATIKA MAABUDU:
YOHANA 4:21-24; 21.Yesu akamwambia, mma, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamuabudu Bba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. 22.Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. 23.Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamuabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Kama umeokoka na hauja mpokea Roho, tafadhali mwombe Mungu akujashe Roho Mtakatifu ili upate kuwa na msaidisi.