Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Damu ya Yesu ina nguvu sana na umuhimu mkubwa katika maisha yetu.
Maandiko kwenye biblia katika kitabu cha WAEBRANIA 9:22; "Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo".
Nataka kusungumzia "POINTI NNE YA UMUHIMU WA DAMU YA YESU"
1.DAMU YA YESU UKOMBOA;
a.Maana ya neno ukombozi:- Ni kununua tena ama kuokoa kwa kulipia fidia.
b. Neno fidia ya manisha:- Bei inayo lipishwa ili mtu aondolewe kwenye mateka.
Sasa damu ya yesu ndiye fidia iliyo lipwa kwa ajili ya ukombozi wetu. Ndiyo maana Kitabu cha YOHANA 3:16 yasema; Kwa maana jinzi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, baliawe na uzima wa milele. Kahivyo Yesu alitumua na Mungu Baba ili aokoe na kukombowa.
1 PETER 1:18-19; Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fetha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mliyoupokea kwa baba zenu, bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na mawaa, yaani ya kristo.
WAEBRANIA 10:4:- Maana haiwezekani damu ya mafahali na Mbuzi kuondoa dhambi.
2. DAMU YA YESU INASUNGUMZA
WAEBRANIA 12:24; Na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili
a. Inanena UPONYAJI; ISAYA 53:5:- Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
b. Inanena BARAKA. WAGALATIA 3:13; Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti
3. DAMU YA YESU UTUPATANISHA NA MUNGU
Dhambi ilitutenganisha na Mungu, ndiyo maana Isaya 59:2 inasema; Lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone hata hataki kusikia. Mungu anachukia dhambi, ijapo anatupenda sana na ndiyo maana alimtuma Yesu mwanawe wa pekee ili atupatanishe na Mungu kupitia damu yake ya dhamana
a. WAKOLOSAI 1:19-20, Kwa kuwa katika yeye alipendeza utimilifu wote ukae; na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake;kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.
b. WARUMI 5:10, Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya mwana wake; saidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.
Tukidumu katika dhambi, uhusiano kati yetu na Mungu inaharibika, kwa sababu Mungu anachukia dhambi, baali tunapo okoka, Kristo kwa damu yake utukomboa na kurejesha uhusiano mema kati yetu na Mungu, kwa kuwa Mungu ana tupenda. Kwa hivyo damu ya Yesu ina umuhimu kubwa sana katika maisha yetu, kwa hivyo damu ya bwana wetu Yesu ina nguvu na uwezo ya kufanya hayo yote.
Amen, shalom.