Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Katika kitabu cha Wakorintho wa pili mandiko inasema; Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ilininyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;
Paulo mitume anatuhimiza ya kwamba Mungu aweza kutujaza neema kwa wingi, hi inamana ya kwamba, maisha tunayoishi, tunaishi kwa neema, bila neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hatuwezi kufaulu maishani mwetu na vyote tufanyalo, haliwezi kufanikiwa bila neema yake Kristo.
1 Wakorintho 15:10, inasema; Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.
Paulo mitume anasema ya kwamba jinzi alivyo ni kwa neema, na hiyo neema imemuwezesha kufanya kazi kwa bidi. hili ujumbe wa Paulo inatufunza ya kwamba ukifaulu maishani usijivune na kupiga kifua kwamba ni uwezo wako, ama akili yako, ama bidi yako, ama masomo yako, ila ni kwa neema yake Mungu.
katika kitabu cha PETERO wa pili, mandiko yasema; Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.
WAEFESO 3:7-8; Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake. (8) Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri mataifa utajiri wake Kristo usiopimika.
YOHANA 1:16; Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.
Tunaishi kwa neema, chochote tufanyacho, tufanye kwa neema.