Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Luka 16:19-31
Huu ni hadithi ya watu wawili kwenye biblia, mmoja aliitua Lazaro, mwingine akaaitwa tajiri. Biblia inasema, tajiri huyo aliishi maisha ya anasa, bali lazaro alipitia mateso lakini hata hivyo, aliishi maisha matakatifu. Katika mlango wa 22; inasema, ikawa yule maskini (Lazaro ) alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Mlango wa 23-24,inasema; Basi kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia,akasema Ee baba Ibrahimu ,nihurumie ,umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini,auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Katika haya ya 27-28; Akasema, Basi,baba nakuomba, Mitume nyumbani kwa baba yangu. Kwa kuwa ninayo wandugu watano, ili awashuhudie, Washoe was pia wakafika mahali hapa pa mateso.
Hadithi hii inatufuza ya kwamba, hakuna TOBA baada ya kufa, tubu dhambi zako zote ungalipo hai. Ukifa ukiwa hauja tubu dhambi zako, utaenda kusimu mahali pa mateso. Tajiri akamwambia Ibrahimu amtume Lazaro kwa Babake awashuhudie wandugu zake wasiende mahali alipo. TOBA ni sasa ungalipo hai.
Katika biblia, kwa kitabu cha Isaya 55:6-7; Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, mwiteni, maadamu yu karibu. Mtu mbaya na aache njia yake,na mtu asiyehaki,na aache mawazo yake; na amrudie BWANA, naye atamrehemu; na arejee kwa Mungu wetu,naye atamsamehe kabisa.
Basi ninahimiza kila mmjo atakaye soma ujumbe huu popote ulipo, uwe katika nchi za kiafrika, uwe ulaya ,ama merikani. Nakusihi utubu dhambi zako zote na umgeukia BWANA naye atakusamehe. Kwa kuwa MUNGU watu amejawa na Rehema na neema tele.