Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Wapendwa wangu, Mungu baba kupitia Roho Mtakatifu ametia ujumbe huu ndani yangu ili nikaweze kuushiriki pamoja nawe. Chochote ufanyacho katika mwili wa Kristo Yesu si bure, baali utalipwa na baba wetu Mungu wakati utakapofika. waliyo okoka lazime wawe na kazi ya kufanya katika mwili wa Kristo; Iwe ni maubiri, au uinjilisti, ama kuongoza sifa kanisani, Iwe ni kutumikia Mungu kwa maali yango, ama kazi ya uzimanzi, na mengine mengi. Kila atendaye kazi atalipwa, na malipo yetu yaanzia hapa duniani, kisha baada ya kuondoka duniani, Mungu atatupa thawabu kule Mbinguni baada ya kumaliza kazi duniani.
Paulo Mitume anawaandikia kanisa la korintho akiwatia moyo kwa kila kazi wanayo fanya katika mwili wa Kristo akiwambia katika 1 Wakorintho 15:58 akiwambia "Basi, ndugu zangu wapendwa , mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kaziya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana".
Naye katika kitabu cha Wakolosai 3:23, mandiko yasema; "Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu", Paulo mitume ana waandikia kanisa akiwaambia ya kwamba, kila kazi wanayo fanya katika mwili wa Kristo, wafanye kwa Roho bila kumwangalia mwingine hata kama ni mkubwwa wako, usiweke mawazo yako kwa mwanadamu, maana chochote ufanyacho katika mwili wa Kristo, ni Kristo mwenyewe ata kulipa, wala si Mwanadamu.
Kitabu cha Waibrania 6:10 inasema; Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolithihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia.
Ili upoke thawabu, lazima utatia biidi pasipo kuchoka, watu wengi walianza vizuri na hata sasa wametia biidi, na hivi karibuni, utavuna ulicho panda. So tusichoke. Wagalatia 6:9 inasema; " Tusichoke kwa kutenda meema, kwa kuwa Siku ikifika.