Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Mwanzo 1:26; MUNGU akasema, na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
kulingana na huu mandiko katika kitabu cha Mwanzo, Roho Mtakatifu alikwepo pamoja na Kristo na Mungu kabla ya maumbile kuanza, na pia alishiriki katika uumbaji.
Roho Mtakativu pia upatiana uhai, na ndio maana mandiko yasema katika kitabu cha YOHANA 6:63; Roho ndiyo itiayo uzima , mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima
AYUBU 33:4 Inasema; Roho ya MUNGU imeniumba, na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai
Kwahivyo baadhi ya kazi za Roho Mtakatifu ni uumbaji na kupatiana uhai
< > Roho Mtakatifu ni utu tofauti, baali sio nguvu binafsi ama nguvu tu za kawaida ambayo tunaweza kutumia jinzi tunavyo taka.
Roho Mtakatifu ni Wakili; JOHN 15:26- Lakini ajapo huyo msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa baba, yeye atanishuhudia.
Roho Mtakatifu ni MFARIJI; YOHANA 14:26; Lakini huyo msaidizi, huyo Roho mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote na kuwafundisha yote niliyowambia
Roho Mtakatifu ni MUOMBEZI; WARUMI 8:26; Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkua.
Ninaomba ukaweze kumkubali Roho Mtakatifu aingie ndani yako awe msaidizi wako.