Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo ina maana kuu sana kwa maisha yetu. Sisi zote tunaokolewa kwa kuamini ya kwamba Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi, kisha siku ya tatu akafufuka kutoka kwa waafu.
1 Wakorintho 15:1-4, maandiko yasema "Huu ndiyo injili tunayo ubiri, na mtu anapo amini, ataokolewa na kufanyika muumini katika Kristo Yesu"
Hii ina maana kwamba, kifo cha Yesu Kristo ina nguvu inayo leta wokovu.
Katika kitabu cha Waefeso 1:13-14, kwenye haya ya 13"Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye mtakatifu."
Katika haya ya 14, maandiko yasema; " Ndiye aliye arabuni ya uridhi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake" Mtu anapoamini kwa Yesu Kristo na kuokolewa, utiwa muhuri la Roho mtakatifu, kisha anapewa ulinzi tosha, popote aendapo anaalama ya muhuri la Roho Mtakatifu ambayo inadhihirisha ya kwamba yeye ni mwana wa Mungu. Ndiyo maana neno la Mungu linasema kwa kitabu cha Yohana 1:11-12; Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.
Na kwa kitabu cha 2Wakorintho 5:17, maandiko yasema; Hata imwkuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! yamekuwa mapya.
"Kuna jinzi mbili ningelipenda tujifunze kwa hili ujumbe"
Jinzi ya kwanza;
Ni kwamba Kristo Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, na tunapo amini hivyo, tunakubaliana na Mungu ya kwamba kweli sisi tu wenye dhambi na tunahitaji Mwokozi ili tuweze kutubu dhambi zetu na kuokolewa.
Jinzi ya pili;
Ni kwamba Yesu Kristo alipo fufuliwa kutoka kwa wafu, tulifufuliwa pamoja naye, na sasa hatuko kwa kifungo cha dhambi inayoleta mauti, baali tu hai pamoja na Yesu Kristo. Na uhai wetu umefichwa kwa Yesu Kristo. Warumi 6:4; "Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima".
Je mpendwa wangu, ungelipenda kutoa uamuzi gani? Je unaweza kumwamini Kristo Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako?