Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Je! wajua ya kwamba unapo okolewa na kuwa muumini katika Kristo Yesu, Mungu anakupatia nafasi nyingi za uridhi katika Ufalme wake, hii ni kwa sababu ya uhusiano mpya kati yako na Christo Yesu kupitia wokovu (1Korintho 15:1-4).
Tunapata ukombozi kupitia damu ya Yesu Kristo na msamaha ya makosa yetu yote kulingana na wingi wa neema ya Mungu ambayo ameiachilia juu yetu kulingana na upendo wa ajabu alilotupenda kwalo. "Waefeso 1:7-8 Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu , masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake. 8. Naye alituzidishia hiyo katika hekima yote na ujuzi".
Tumepata urithi yakiwa yamekusudiwa kulingana na mipango yake Mungu ya kwamba tubatilishwe katika mfano wake Kristo Yesu(Warumi 8:29, Waefeso 1:11, 1 Petro 1:3-5)
Tume hesabiwa haki na kutakaswa katika Kristo Yesu (Warumi 5:1, 8:30, Wagalatia 2:16, Tito 3:7, Matendo ya Mitume 20:32, 26:18, 1 Korintho 1:2,30, 6:11, Wahibrania 10:10,14)
Tumetiwa muhuri katika Kristo Yesu kwa Roho Mtakatifu tulipoamini kwa Injili.(Waefeso 1:13-14, 4:30)
Tumefanywa viumbe vipya katika Kristo (2 Korintho 5:17)
Mungu ametuinua juu na kutuketisha na Kisto Yesu ili tutawale pamoja naye Mbinguni (Waefeso 2:4-6)
Kwahivyo ni mapenzi yake Mwenyezi Mungu sisi zote baada ya kuamini Injili takatifu, kutembea kwetu na Kristo Yesu idhihirishe sehemu yetu wa urithi katika ufalme wa Mungu (1 Wakorintho 15:1-4)
ENDELEA KUTAZAMIA JUU (Tito 2:13)