Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Aketiye mahali pa siri pake aliye juu. Atakaa Katika uvuli wake Mwenyezi.
Nitasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.
Maana yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, na katika tauni iharibuyo
Kwa manyoya yake atakufunika, chini ya mbawa zake utapata kimbilio. Uaminifu wake ni ngao na kigao
Hutaogopa hofu ya usiku, wala mshale urukao mchana, wala tauni ipitayo gizani, wala uele uharibuyo adhuhuri
Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume. Hata hivyo hautakukaribia wewe. Zaburi 91:1-7