Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
METHALI 4:23
maandiko yasema kwamba; linda moyo wako kuliko yote uyalindayo.
Wapendwa moyo ni sehemu muhimu sana katika maisha ya wanadamu, maana yote unayo yaona ikitendeka kwa inche utoka kwa moyo. Kwahivyo chochote mtu afanyacho utoka kwa moyo. Ndio maana mandiko yasema linda moyo wako.
Katika kitabu cha LUKA 6:45 inasema; mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake utowa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinyua chake hunena yale yaujazayo moyo wake.
Moyo ikijaa mambo yaliyo mema, unayo ya tamka kinyuani mwako yatakuwa mema, moyo ukijaa ukarimu, utakuwa mkarimu, moyo ukijaa yaliyo mema, matendo yako yatakuwa mema. Lakini ikiwa moyo wako utajaa na yaliyo maovu, matendo yako yatakuwa maovu, moyo wako ukijaa matusi,kinyua chako yatanena matusi. Chochote yanayo onekana kwa inje, utoka kwa moyo. moyo ikijaa dhambi, utatenda matendo ya dhambi, lakini ukijaa haki utakuwa mwenye haki mbele ya mwenyezi MUNGU. Mpendwa, linda moyo wako kuliko yote uyalindayo.
ZABURI 51:10 Daudi akamsihi Mungu akisema; Ee MUNGU, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu.Haya ya 11; Usinitenge na uso wako, wala Roho yako mtakatifu usiniondolee. Roho ya Bwana uishi mahali patakatifu, hawesi kuishi mahali pa chafu, Kwahivyo ukichafuka moyo, Roho mtakatifu ataondolewa. Hivyo basi, linda moyo wako usije ukaujaza na maovu.
Naomba mwenyezi MUNGU akuumbie moyo mpya, moyo uliyo safi katika jina la YESU, amen.
by John Joachim// Zilizowekwa 05 Machi 2021// Bendera kama haifai // Jibu // Ghairi jibu
by Maro Sylvester// Zilizowekwa 19 Juni 2021// Bendera kama haifai // Jibu // Ghairi jibu
by Blessing Charles// Zilizowekwa 26 Juni 2021// Bendera kama haifai // Jibu // Ghairi jibu