Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Kuweka matumaini yetu kwa Kristo, ni kuamini kwake Kristo ya kwamba yeye peke anauwezo juu ya maisha yetu.
1John 3:1-3
Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.
Mmoja ya matokeo ya kuweka matumaini yetu juu ya kuonekana kwa Mwokozi wetu Yesu Kristo, ni tamanio la kuishi maisha ya usafu, maisha inayo mpendeza Mungu.
Tito 2:13-14.
Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe , wale walio na juhudi katika matendo mema.
Tuna wakati ujao mtukufu unaotungoja katika Kristo. Siku mmoja karibuni, tutakuwa pamoja na Bwana wetu Yesu Kristo na tutamwona uso kwa uso jinzi alivyo.
Mungu awabariki sana, na muendele kumtumainia Bwana wetu Yesu Kristo. AMEN