Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
1 Wakorintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Tunapo mpokea Kristo kuwa bwana na Mwokozi wetu na kukaa ndani ya Kristo, Mungu anatufanya kiumbe kipya yaliyo matakatifu, mtu wa kale na maisha yake ya dhambi uondolewa, tazama yote yanakuwa mapya.
Kufanywa kiumbe kipya hayatokani na kazi njema tunayo fanya, bali ni sehemu ya wokovu tunayo pokea kwa Kristo Yesu aliye tununua kupitia damu yake iliyo mwagika Kalvari, hiyo damu inatufanya upya siku baada ya siku.
1 Wakorintho 2:14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinzi ya rohoni.
Tumepatiwa wazo mpya ambayo kilamara inawaza mambo yanayo ambatana na maisha yetu mapya bali siyo kiumbe yetu ya kale. Kwahivyo kama viumbe vipya, tunastahili kuweka mawazo yetu kwa mambo ya rohoni. Roho mtakativu hutuongoza kuyawaza mambo mapya yanayo ambatana na mawazo yetu mapya kwa kuwa tu viumbe vipya.
Wagalatia 5:16 inasema; Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtatimiza kamwe tamaa za mwili.
Tunapo enenda kwa Roho, mtu wetu wa ndani ataendelea kutiwa upya, wala hatutatimiza mapenzi ya mtu wa kale (mwili).
Nawasihi wapendwa, tukaye ndani ya Kristo ili tuweze kuishi maisha mapya inayo mpendeza Bwana wetu Kristo Yesu.