Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Upako wa Roho Mtakatifu, ni nguvu ya Kimungu inayo tuwezesha kufanya kazi isiyo ya kawaida. Upako inatuwezesha kufanya yale mwili haiwezi kufanya.
1 Samueli 16:13; Ndipo Samueli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake;na roho ya BWANA ikamjia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samueli akaondoka, akaenda zake Rama.
Daudi kijana mdogo wa Jese alikuwa alikuwa mchungaji wa mifugo ya babaye, lakini baada yakupakwa mafuta na Samueli, Biblia inasema, Roho ya BWANA ikaja juu yake kwa nguvu. Baada ya kupokea upako wa Roho Mtakatifu, Daudi akamwelekea mfilisti aliyekuwa akiwateza wana wa Israeli, akamuuwa kwa jiwe, (1 Samueli 17:45-50).
Hatuwezi kufanya lolote pasipo Roho Mtakatifu anaye tutia nguvu kutokana na Upako wa Roho. Waubiri wanaitaji upako wa Roho Mtakatifu, wanayo mwabudu wanaitaji upako wa Roho mtakatifu, wanao tumikiwa na Mungu kupitia kipawa cha mujiza na uponyaji, wanapata nguvu kupitia upako wa Roho Mtakatifu. Hakuna aliye na uwezo ya kufanya kazi kisicho cha kawaida, ila kwa upako wa Roho Mtakatifu. Yesu akawambia wanafunzi wake katika kitabu cha "Matendo ya mitume 1:4; Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali wangoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu". Yesu alimanisha kuja kwa Roho Mtakatifu(Matendo ya mitume 2:1-4). Wanafunzi wa Yesu hawangeweza kuendelea na kazi ya kuubiri baada ya Yesu Kristo kutualiwa, ndiyo mana Yesu anawaambia waende Yerusalemu wamgojee Roho Mtakatifu atakaye watia nguvu ya kuendelea na kazi ya uduma.
ILI UPOKEE UPAKO WA ROHO MTAKATIFU, LAZIMA UOKOKE NA UJAZWE ROHO MTAKATIFU.
Mathayo 9:17; Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikaifadhika vyote
2 Wakorintho 5:17; Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya.
Ukitaka kutembea chini ya upako wa Roho Mtakatifu, lazima uokoke, ujazwe Roho Mtakatifu na ufanyike kiumbe kipya.