Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
MHUBIRI 7:8; "Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake, na uvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi"
Sisi sote tuliyo okoka, tunafananishwa na wanariadha wanayo kimbia mbiyo ya masafa marefu. Tunakimbia tukiwa na matumaini ya kumaliza vizuri na kutunukiwa taji ya uzima.
Maandiko yasema kwa kitabu cha Waebrania 12:1; "Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito , na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu".
WANAYO MALIZA MWENDO VIZURI PEKEE NDIYO WATAPOKEA TUZO
Kila mtu anaye shiriki katika mashindano hufanya hivyo kusudi apokee taji, nasi tunaye kimbia mbiyo ya imani, twafanya hivyo kusudi tupokee taji ya uzima. Kwahivyo sisi zote tuliye okoka, tuko mbiyoni, na tusipo choka na tumalize salama, Kristo Yesu atatufaliza taji ya uzima.
1 Wakorintho 9:24-25; "Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote . lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate. Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo ; bali sisi tupokee taji isiyoharibika"
Isaya 40:29,30 na 31; "Haya ya 29; Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo".
Haya ya 30; "Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka".
Haya ya 31 "Bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu wala hawatazimia."
Wafilipi 3:13-14; "Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele. Nakaza mwendo , niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu."
Wapendwa tukase mwendo, tusicho, tukifahamu ya kwamba, taji yetu yatungojea. Hakuna yeyote ambaye ameokoka na anamtumikia Mungu kwa uaminifu ambaye Mungu amekosa kumbariki.