Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Sisi zote tulio okoka, tu kama wakimbiaji wa mbio za masafa marefu. Tunakimbia tukiwa na matumaini ya kumaliza visuri.
Katika maandiko kwenye kitabu cha Mhubiri 7:8 inasema; Heri mwisho wa jambo kuliko mwanzo. Hilo maandiko inatufundisha ya kwamba; haijalisi jinzi umeanza mwendo, kilicho cha maana ni jinzi utakavyo maliza. Nataka nikutie moyo mpendwa, kengele iko karibu kulia ambalo ni ishara ya kumaliza mwendo, je kengele ikipigwa leo hii utamaliza vipi?, utapata tuzo ama utakosa? Tuzo watapewa walio maliza mwendo vizuri peke yao.
Katika kitabu cha Waebrania 12:1-2, kwenye msitari ya 1 inasema; Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu. Katika msitari wa 2, inasema; tukimtazama Yesu , mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.
Wapendwa dunia sio kwetu, kwetu ni mbinguni, na tuko mbioni tukitazamia kumaliza mbio salama ili tuungane pamoja na wenzetu walio maliza mwendo mbele yetu, katika kitabu cha Wafilipi 3:20 inasema; Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni ; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi Bwana Yesu Kristo.
Mwendo huu sio raisi, wengine walioanza vizuri, wamemaliza vibaya. Wengine walianza kwa bidii, leo wamekuwa wanyonge, wengine walianza kwa moto, leo hii wamekuwa vuguvugu. Wengine walianza wakiwa hodari kwa maombi, leo hii, wamelemewa, hawawezi kuomba hata dakika kumi. Mbio umekuwa mgumu sana, wengine wameacha mbio kwa katikati. Nakuombea mpenwa, Mungu akutie nguvu ili upate kuendelea mbele na mbio. Isaya 40:30-31; Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. Isaya 40:29; Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
Wafilipi 3:13-14 Paulo anasema; Ndugu, siijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika ; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele. Nakaza mwendo, niifikilie mede ya dhawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. Sahau yaliyo nyuma, sahau maisha ya anasa ulioishi, sahau maisha ya ulevi ulioishi, tazama mbele na uendele na mbio, dhawabu yakungojea mpenwa, tia bidii usichoke, Mungu atakutia nguvu. Natusisahau jambo hili, wenye watamaliza visuri na kupata taji, ni wale wameokoka pekee yao, hakuna taji kwa wenye dhambi. Kwahivyo kama hauja mkiri Bwana Yesu kuwa mwokozi wa maisha yako, tafadhali okoka ili umalize mwendo vizuri.