Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Kusudi kuu ya kuja kwake Yesu ulimwenguni kwa mara ya kwanza ilikuwa kwa ajili ya; Kuokowa na kukomboa mwanadamu kutoka katika utumwa wa dhambi.
< > WARUMI 6:23, Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; baali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
< > YOHANA 3:16, Kwa maana jinzi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele
Kusaliwa kwa Yesu Kristo ili tabiriwa na nabi Isaya; " ISAYA 9:2,9, haya ya 2; Watu wale waliyokwenda katika giza wameona nuru kuu; wale walioka katika nchi ya uvuli wa mauti, Nuru imewaangaza. 6. Maana kwa ajili yenu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanaume, Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake, mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.
Naye Mathayo anasema ya kwamba Mwana anaye zaliwa, atapewa jina Emmanuel, yaani Mungu pamoja nasi MATHAYO 1:23
HUYU YESU KRISTO aliye zaliwa ni nani?
Yeye ndiye mwokozi; "MATENDO YA MITUME 4:12, Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu waliyopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo"
Yeye ndiye mwanga wetu; "YOHANA 1:4-5, Haya ya 4.Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. 5. Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.
YOHANA 8:12, "Basi Yesu akamwambia tena akasema, mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima"
Yeye ndiye mchungaji wetu; "YOHANA 10:11, Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. "ZABURI 23:1, 4; 1. Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. 4. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya; kwa maana wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji"
Mpendwa, jinyenyekeshe na ujikabidhi kwa Bwana wetu Yesu Kristo ili akuondole mizigo zote, akuponye magonjwa yote, akusamehe dhambi zako zote, akukomboe na akutakaze kwa damu yake iliyo mwagika msalabani.
Shalom, Mungu akubariki sana kwa kuwa mnyenyeke na kusoma ujumbe huu, endelea kutazamia Kristo Yesu, mwanzilishi na mkamilizi wa imani yetu.