Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Wengine wetu kama si neema, hatunge kuwa jinzi tulivyo. Matendo yetu yalikuwa maovu sana, lakini kwa Neema yake Yesu Kristo, tumeokolewa na kukombolewa kwa damu ya Yesu Kristo. Mungu aliyejawa Neema na huruma nyingi ijapo tulikuwa wenye dhambi zugu, kwa sababu ya upendo wake mkuu kwa watu wake, hata kama tulikuwa waafu katika dhambi zetu, alitufanya kuwa hai pamoja na Kristo kupitia neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.
1 WAKORINTHO 15:10; Lakini kwa neema ya Mungu, nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.
WAEFESO 2:4-5 (V1)Inasema; Lakini Mungu,kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; (V5) hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani tumeokolewa kwa neema.
EFESIANS 2:8-9; (v8)Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafasi zenu, ni kipawa cha Mungu. (v9) wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
Yesu akuita, uje jinsi ulivyo, hana ubagusi, yeyote amkimbiliaye, hawezi kukutupa.
ISAYA 1:18; Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Yesu akuitaji jinzi ulivyo, hata kama wewe ni mfuta bangi, njoo tu jinzi ulivyo, Kristo Yesu anakupenda, ukija kwake, hawezi kukuacha katika dhambi, bali atakusafisa kwa damu ya Yesu.
Tafadhali, njoo jinzi ulivyo