Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
WARUMI 12:1-2 Inasema;
1. Basi,ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo, ibada yenu yenye maana. 2. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii , bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Kwanza, lazima tutoe miili yetu kwa Mungu kama dhabiu yaliyo hai, iliyo tengwa kwa ajili ya kazi ya kiroho. Ina tupasha kudumu ndani ya Kristo ziku zote ili tusiweze kuishi maisha ya kiulimwengu, bali maisha matakatifu inayo mpendeza Mungu.
Katika hicho kitabu cha Warumi mlango wa 12 kwenye msitari wa 2; Inatuambia ya kwamba, Tusiifuatishe namna ya dunia hii, bali tugeuzwe kwa kufanywa upya nia zetu. Kugeuzwa nia zetu, inamanisha, nia zetu inafa kuelekezwa kwa njia za Mungu na kuanza kufanya mapenzi yake Mwenyezi na kujitolea mwanga kumuishia Yesu Kristo.
2 WAKORINTHO 5:17 Inasema;
Hata imekuwa, mtu akiwa ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; yakale yamepitatazama! Yamekuwa mapya.
Hii inajumuhisha kufanywa upya kwa mawazo yetu ya kiroho. Ila tu kila muumini anayo chaguo la kufanya kwa hili jambo. Kila mtu anayo uhuru wa kuchagua aidha kutii maagizo haya na kuamua kubadiliswa kwa njia ya kutiwa upya nia zao, ama kugairi maagizo na kusalia kwenye nia zao mbaya inayo waongoza katika njia za uharibifu. Kwahivyo, hii inamanisha, waumini katika Kristo wanaeza kufuatisha namna ya dunia hii ama wanaeza kubadilishwa kwa nia zao ili wafanyike dhabiu iliyo hai kwa Mungu. Kwahivyo uamuzi ni wa kila muumini kuchagua ni ulimwengu gani ya kuishi, aidha kuishi katika ulimwengu wa kiroho ama ule wa kimwili.
Katika nakala hii, ninanena na waumini katika Kristo, kama kweli wewe ni muumini katika Kristo, na umekubali kufuata maagizo hayo yote, wokovu wako utakua wa dhamana sana wala hakuna kitakacho tutenganiza na upendo wa Mwenyezi Mungu (WARUMI 8:38-39)
Endelea kutazamia juu kwenye kiti cha enzi.