Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Katika biblia kitabu cha Waibrania 11:1 maandiko yasema kwamba; Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Katika waibrania 6:6 maandiko yasema; Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba huwapa dhawabu wale wamtafutao.
Ni vyema kuishi na kutembea kwa imani, maana pasipo imani hatuwezi kumpendeza Mwenyezi Mungu. Popote Yesu Kristo ilienda akiponya wagonjwa, aliwambia aliyo waponya; enenda kwa amani, imani yako imekuponya. kwahivyo imani inauwezo ya kuumba mambo yasiyo kuwa na ikawa.
Hata hivyo, ni vizuri kuweka imani katika matendo, hata mandiko inasema ya kwamba kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. Kwa maneno mengine, Ibrahimu alichukua atua ya kuweka imani kwa matendo, akaondoka.
Yakobo 2:14 Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! ile imani yaweza kumwokoa?
James 2:17-18; Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. Lakini mtu atasema, wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo.
Wacha tuweke imani yetu katika matendo.