Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Katika WAFILIPI 2:19-21, Inasema;
19.Walakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu. 20.Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli. 21,Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu.
Tunapo jifunza neno la Mwenyezi Mungu, ni viema tukumbuke ya kwamba watu kama Paul, Petero na Yohana hawakupitia majaribio kutoka inje bali mpaka wandani wake. Palikuwa na waumini ambayo hawakuwa wakitafuta vitu vya Bwana, bali walimfanya Paulo awe katika hali mgumu wa kuhubiri. Kwa njia hiyo hata sasa kuna watu wengi kanisani ambayo hawaendi kanisani kutafuta namna watakayo uridhi uzima wa milele, bali wanatafuta vitu itakayo wa faidi hapa duniani; wengine wanatafuta miujiza badala ya kumtafuta Yesu Kristo na ndiyo sababu waubiri wa uwongo wametokea wengi na kufanya miujiza za uwongo.
Mmoja ya mtu wa maana kwa wale waliomuacha Paulo ni msirika wake aitwaye Demas. Na walikuwa na Pulo kule Roma.
WAKOLOSAI 4:14 Inasema; Luka, yule tabibu mpendwa, na Dema , wanawasalimu.
Lakini badaye . Dema akamwacha Paulo, hili jambo Paulo ameutaja katika kitabu cha TIMOTHEO WA PILI 4:10 akisema; Maana Dema aliniacha. akiupenda ulimwengu huu wa sasa, akasafiri kwenda Thesalonike; kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda Dalmatia.
1 TIMOTHEO 6:12 inatuambia; Piga vita vile vizuri vya imani, shika uzima ulewa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashaidi wengi.
WAEFESO 6:10 Inasema; Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
WAGALATIA 6:10 pia inatuambia; Kwahiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote wema; na hasa jamaa ya waaminiyo.
Naye kitabu cha WAFILIPI 1:6 inasema; Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kasi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu.
Mungu awabariki na tuendele kutazamia Mbinguni.