Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Watu wengi wangelipenda kumjua YESU. Na mara nyingi watu wajiuliza maswali mengi; Huyu YESU ni nani? YESU ni mwana wa Mungu na pia ni Mungu, yeye ni Mwokozi, mkombozi na mponyaji, na pia ni baba yetu.
YESU ni mwana wa Mungu na ni Mungu na anakaa katika neno lake. Kama vile maandiko kwenye bibilia yanavyo eleza katika kitabu cha Yohana mlango wa kwanza aya ya kwanza; hapo mwanzo palikuwako neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. YESU ndiye neno na mtu anapo pokea neno na kuliamini, atakuwa ame mpokea Yesu.
YESU ni mwokozi, kwa kitabu cha warumi mlango wa tatu aya ya ishirini na tatu, bibilia yasema; kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. YESU alikukuja ulimwengu ili awaokowe wanadamu kutoka kwa utumwa wa dhambi. Yohana3:16 inasema kwa maana jinsi hii, Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. YESU aliacha utukufu mbinguni, akaja duniani, akatembea kati ya wanadamu, aliyafumilia matezo makali kwa ajili yetu ili atuokoe sisi tuliye kuwa waasi. Tito 3:3-6. Na haya ndiyo aliyo yanena malaika Gabrieli katika kitabu cha Luka 2:11 akisema; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.
YESU ni mkombozi. Neno ukombozi ina maana, kununuliwa kwa kulipa garama. Kristo Yesu alilipa garama kwa damu yake aliyoimuaga msalabani ili atukomboe kwenye utumwa wa shetani. Katika kitabu cha Waefeso 1:7 inasema; katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu ,msamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake. Hakuna aliyekuwa na uwezo ya kutukomboa, wala malaika ama mtu awaye yeyote. Ila ni Yesu peke yake iliye weza kumwaga damu ili atukomboe, 1 Petro 1:18-19. Na kwakuwa Bwana YESU alikwisha kulipa garama na akaninunua kwa damu yake ya dhamana, sasa maishani ninayoishi na ishi kwa imani Wagalatia 2:20. Naye Paulo awaandikia Wakolosai barua akiwambia; Naye alituokoa Katika nguvu za giza ,akatuhamisha na kutuingiza Katika ufalme wa mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani msamaha wa dhambi Wakolosai 1:13-14