Inaweza kuhaririwa na kuhariri ukurasa kutoka kwa jopo la kudhibiti
Wapendwa, wandugu na wadada katika kristo Yesu, ningependa ni kuhakikishie kuwa kuna faida mengi yanayotokana na "kukiri". Chochote unacho kiri kwa kinywa chako ndicho Mungu atakutendea.
Katika kitabu cha Yakobo 5:16, mandiko yasema kwamba; Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
Kwahivyo, kuna faida ya uponyaji kwa kukiri. Mungu asikii maombi ya wenye dhambi, ila yeye husikia maombi ya wenye haki(Methali15:29). Kwahivyo, labda umeteseka kwa ugonjwa fulani, umejaribu matibabu mbali mbali, lakini ujapata uponyaji. Nataka ni kuakikihsie ya kwamba Mungu ndiye aponyaye, lakini mpaka ungame dhambi zako kwanza ili uwe na uhuziano mwema na Kristo ndiposa aweze kusikia kilio chako. Kama vile mandiko yasema kwa kitabu Isaya 59:1-3; Msitari wa 1.Tazama Mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata liziweze kusikia. Ndungu na dada yangu, ebu jioji kwa moyo wako, je kuna jambo lolote ambalo lita zuiya mkono wa BWANA wetu asikuponye?
Tukiziungama ndambi zetu,yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote(1 yohana 1:9), Kuna msahama wa dhambi tunapo kiri.
Faida nyingine ya KUKIRI ni "fanaka", Hauwezi kufanikiwa maishani wala kubarikiwa na Mungu ukiwa mwenye dhambi, mpaka utakapo kiri na kutubu dhambi zako zote.(Methali 28:13)
Ili upoke kipawa cha Roho Mtakatifu, lazima utubu dhambi zako na kukiri Kristo Yesu kuwa BWANA na mwokozi wako na upoke ubatizo wa majii mengi. Maana Roho Mtakatifu uka mahali patakatifu, kwahivyo uki ungama dhambi zako, nakubatizwa, utajazwa Roho Mtakatifu ambaye upeana kipawa. Kwahivyo, Kipawa cha Roho Mtakatifu ni faida ya KUKIRI.(Matendo ya Mitume 2:38)
Mpendwa wangu, ningelipenda nikuambie ya kuwa kuna faida mengi sana kwa kukiri na kuungama dhambi zako, ukiokoka na kukaa ndani ya Kristo, unafanyika kuwa kiumbe kipya, mambo ya kale upita (2Wakorintho 5:17). Naomba Mungu wa amani akusaidie na aweze kuguza moyo wako ili uweze kutubu dhambi zako na umpokee Kristo Yesu kuwa BWANA na Mwokozi wako. Maana ukimpokea BWANA YESU, atakufanya kuwa mwana wa MUNGU.(Yohana 1:12).
Baada ya kusoma nakali hii, na umesawizika moyoni ya kuwa ungelipenda kukiri na kutubu dhambi zako, ningelipenda uombe hili ombi;
Bwana Yesu, nimesawizika moyoni, yakuwa mimi ni mwenye dhambi, ninakiri dhambi zangu zote, Baba nisahamehe makosa yangu yote, nisafise kwa damu yako, unitakaze moyo, asante kwa kuniokoa, kwajina la Yesu Kristo nimeomba na kuamini, AAAAMEN.