Isaya 55:6-7; Bibilia inasema, mtafuteni BWANA maadamu anapatikana, mwiteni, maadamu yu karibu; mtu mbaya na aache njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo yake, na amrudie BWANA. Naye atamrehemu; na arejee kwa Mungu wetu, naye atamsamehe kabisa.
Hili ni agizo lake Mungu, anatoa maonyo kwa watu wote kwa kila taifa ya kwamba tuache njia zetu zote maovu, na tuweze kumrudia tukitubu dhambi zetu zote. Anasema ya kwamba tumtafute maadamu anapatikana. Inamanisha ya kwamba toba ni sasa hivi, maana hajui wakati Bwana Yesu atakapo rudi.
Katika kitabu cha 2 Petro 3:9 biblia inasema; Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, baali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee,bali wote wafikilie toba.
Huu ni mwito wake Mungu kwa watu wote watakao sikia sauti hii, tafadhali popote ulipo, uwe ni mama,mzee ama kijana. Ebu jioji moyoni mwako, ikiwa kuna njia moja ama nyingine umemtenda Mungu dhambi, tafadhali ni wakati wako umtafute Bwana Yesu maadamu anapatikana, uka weze kutubu dhambi na kumgeukia Mungu.