Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. Waliozaliwa, si kwa damu wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
Hapo mwanzo palikuwako Neno, nayoe Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Naye nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.