Bwana u sehemu yangu, rafiki yangu wewe,Katika safari yangu tatembea na wewe. Pamoja na wewe, pamoja na wewe Katika safari yangu tatembea na wewe.
Mali hapa sikutaka, ili ni heshimiwe na yanikute mashaka sawa sawa na wewe. Pamoja na wewe pamoja na wewe heri nikute mashaka, sawasawa na wewe.
Niongoze safarini, mbele unichukue, mlango kwa mbinguni, niingie na wewe. Pamoja na wewe, pamoja na wewe, mlango kwa mbinguni niingie na wewe.
Nionapo amani kama shwari, ama nionapo shida; kwa mambo yote umenijulisha, ni salama rohoni mwangu.
Salama rohoni, ni salama rohoni mwangu
Ingawa shetani atanitesa, nitajipa moyoni kwani. Kristo ameona unyonge wangu, amekufa kwa roho yangu.
Dhambi zangu zote wala si nusu, zimewekwa msalabani; wala sichukui laana yake. Nisalama rohoni mwangu.
Ee Bwana himiza siku ya kuja, panda itakapolia, utakapo shuka sitaogopa, ni salama rohoni mwangu.