Neno la Mungu lina nguvu, uwezo na mamlaka. kuanzia kitabu cha mwanzo hadi ufunuo limejaa neno. Kuna tofauti kati ya maneno na Neno; maneno ni ya mwanadamu, ila Neno ni la Mungu.
Mahali pa muhimu kuka ni katika uwepo wa Mwenyezi Mungu, Hilo ndilo siri ambayo Daudi aligundua, Daudi alidumu uweponi pa Mwenyezi Mungu. Kwahivyo tukidumu katika uwepo wa Mungu, tutakuwa salama.
Silaha ni chombo kilichoundwa kwa ajili ya vita, na inatumika kwa ajili ya ulinzi na kukabiliana na maadui. Kwenye fasiri la kingeresa ukisoma hilo kitabu cha YEREMIA 51:20 katika toleo la mfalme Yakobo, inasungumza kuhusu SHOKA.
TOBA ni nini? Toba ni kuacha matendo mabaya na kuanza kutenda mema, ama ni tendo la kubadilisha mawazo ya mtu kutoka kwa matendo ya uovu na kumgeukia Mungu. Kwahivyo inamanisa toba ni utaratibu wetu wakuendelea maishani mwetu.